Simulizi: KUMBUKUMBU KUMBUKIZI.
Mwandishi: KENNEDY NJERU.
Nambari za mawasiliano: 0748369654.
DONDOKA NAYO...
Nipo katika kitanda changu kati ya vyumba vya gereza nikisubiri amri kutoka kwa askari kunifunga minyororo ili kupelekwa kwa miadi ya siku hiyo. Katika gereza lile la kike, kila mwanagereza waliniogopa kwa ubabe niliokuwa nao na jinsi nilivyo mkaidi. Niliongozwa na askari was kike wawili mbele na wawili nyuma wakiwa wamejihamia kwelikweli iwapo nikijaribu kuwashambulia kwa maana ilikuwa mazoea yangu. Askari wale waliniongoza hadi katika chumba kimoja kilichopo cheupe, ndani mlikuwa na vifaa vya zahanatini ikidhibitisha kuwa kilikuwa chumba cha zahanati cha gereza kuu la Kenya la wanawake.
"Daktari, tumepokea maelekezo kutoka kwa mkuu wa gereza ya kumleta mfungwa 604 kwa ajili ya vipimo vya akili," mmoja kati ya askari wale alitoa maelezo yake akimuelekezea daktari aliyekuwa akijitayari kwa vipimo vile. "Asanteni kwa kumleta, munaweza kumsubiria hapo nje," daktari aliyanena maneno yale na kuwaashiria mlango. Muda usio mrefu tulikuwepo mimi na daktari ndani ya chumba kile, nilimtazama kwa macho ya uhasama huku hasira zangu zikinipanda kwa kasi. "Daktari, natumae haujasahau mpango wetu. Nilikupa masaa ishirini na manne uniletee vifaa ambavyo nilikuagiza!" Nilimnongonezea daktari huko bado nimemkazia macho. "Aisha kuwa mpole, kila kitu kinaenda kama tulivyopanga. Mikakati yote ipo tayari na kila mtu yupo katika mstari wa mbele kwa misheni hii. Vifaa vyako hivi," daktari Ahmed alinena huku akinikabidhi kifaa kidogo aina ya ufunguo wa pingu na upande wa mwisho kikiwa na makali ya kisu. Daktari alionekana mwenye wasiwasi alipokuwa akinikabidhi maana macho yake kila Mara yalitua kwenye mlango, akihofia iwepo askari watamkamata akinikabidhi kifaa kile.
Nilikipokea kwa furaha mithili ya kibogoyo kumea jino changa na kulificha ndani ya mdomo chini ya ulimi. Daktari aliwaashiria askari kuwa ameshakamilisha vipimo vyake na kuwa nipo tayari kuondolewa. Safari ya kurudishwa ndani ya chumba changu cha gereza kilianza tena, wakati huo, mawazo yangu yalinipotelea kutoka na jinsi nilivyokuwa na furaha. Leo ndio mwisho wangu humu gerezani, nilijisemea moyoni huku nikitabasamu.
Mida ya saa tatu usiku, askari aliyekuwa zamu ya kulinda na kufanya ziara kwa kila gereza kuhakikisha kuwa kila mfungwa yupo ulikamilika, alianza safari ya kurudi katika afisi yake kwa mapumziko. Nilinyeyuka kutoka kwa kitanda changu kwa bugudha na kuuchomoa ule mpini na kuujaribisha kwenye nyororo zangu na kufaulu kujifungua. Moyo wangu ulijawa na furaha baada ya kufaulu na kujua kuwa muda usio mrefu nitakuwa nimetoka humu gerezani.
Muda wa kupitishia igizo la uwongo kwa nia ya kumteka askari yule. Nilijibwaga chini huku nikiigiza kilio cha uwongo cha maumivu makali na kusababisha wafungwa walio karibu ni kuamka. Kilio kile kilimfikia askari yule, alinyenyuka mbio kutoka kwenye kiti chake huku akiwa amechikia kitita cha funguo za milango ya gereza. Alikuja hadi nilipo chini huku nimejikunyata na kulishikilia tumbo langu kuashiria kuwa nilikuwa nikipitiwa na maumivu ya tumbo. Katika nafsi yangu nilijichekea nikiona kuwa nilifaulu kumpumbaza askari yule. Punde askari yule alipofika na kuufungua mlango wa chumba changu, nilimgeukia na ngumi moja ya uso ambayo ilimsindikiza hadi sakafuni. Niliichukua minyororo ile na kuishindilia kwenye shingo ya askari yule kwa nia ya kumnyonga. Askari yule alisita kwa mara ya kwanza lakini nilimzidi nguvu na mwisho niliuhisi mwili wake ukilema kuashiria kuwa yupo karibu kukata roho. Niliichukua kitita kile cha funguo na kifaa changu huku nikimbadili sare zake na kumuacha uchi wa mnyama na kuzivaa sare zile. Nilichomoka moja kwa moja ili nisiwatie shauku wafungwa wengi kuwa niko katika miadi ya kutoroka. Nilifaulu kutoka kwenye jumba kuu la gereza ikiwa nimebakiza mita hamsini hadi kwa geti kuu, ndipo niliposkia kipenga kikiambatana na kengele ya gerezani ya kuashiria hatari. Hapo nilifahamu kuwa nimegundulika kuwa nipo katika harakati za kutoka jele, nisijue la kufanya, nilijikuta nikianza kukimbia nikiwa na lengo la kufikia geti kuu. Kutazama nyuma, askari zaidi ya sita waliniandama na silaha tofauti wakiwa na nia ya kunikamata.
Baada ya kufaulu kutoka kwa geti kuu, nilipatwa kwa njia panda maana nje mlikuwa msitu mtupu na barabara kuu ilielekea mji mkuu. Niliamua kukimbia kuelekea msituni kwa maana nilitambua kuwa wangenifwata na magari iwepo ningetumia barabara ile na ningekamatwa. Niliapa kuwa askari hawa ata wanifwate wangapi, kwa udi na uvumbi nitahakikisha wasinipate. Askari wale hawakuachia kunikimbia huku wakifwatua bunduki zao kunielekezea. Kisa hiki kilikuwa sawia na Swara afukuzapwo na Simba, na kujaribu kila awezavyo kutorokea kuwa kitoweo Cha Simba. Hasira na uoga vilinifanya nikimbie kwa kasi mno, nao askari wale walivyoona jinsi nilivyokuwa nachomoka mbio nao walijitahidi kunifwata. Katika harakati za kukimbizana za Swara na Simba ikiashiria mimi na askari zilivikia ukingoni. Nilijikuta nikifunga breki za ghafla baada ya kuona nimefikia mwisho wa safari, ulikuwa mwisho na chini ilikuwepo mteremko ulioelekea baharini. Nikitazama nyuma, askari walikuja kwa kasi mno huku wakikwepa miti ambayo ilikuwa vikwazo kwao. Aisha hapo chaguo ni mbili, ukubali kukamatwa na urudishwe jela na kuongezea kifungo au ujirushe baharani kuepukia hilo, ni Mungu tu atajua hatma yako,hayo yalikuwa mazungumzo akilini mwangu. Niliamua kujirusha baharini ambapo ulikuwa urefu wa kilomita moja, jinsi nilivyoteremka uoga na mshtuko viliniparamia kwa pamoja nisijue jinsi ya kutua majini.
Chubwi!....
ITAENDELEA!!!

Good one
ReplyDelete